Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Maabad S. Hoja akifafanua jambo wakati wa kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyopata mkopo kutoka Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Bw. P. Kagimbo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia (MB) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda (Mwenye miwani kushoto) akisisitiza jambo kwa mwanachama wa Kikundi cha Sokoine Youth Development Bw. Swaka Abbas wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Manispaa hiyo jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...