Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukikatiza katika mtaa wa Daraja Bovu wakati wakielekea
kuzindua na kushiriki ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Kiungani. katika
jimbo la Chumbuni,Wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.
Mbunge wa Chumbuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Pereira Ame Silima akizungumza jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto aliposhiriki ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Kiungani.
Mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.Salim Hassan Abdullah Turky akisalimiana
na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakati alipowasili katika jimbo la
Mpendae mapema leo katika wilaya ya Amani Mkoa wa Mjini Magharib,ambapo pia alipokea taarifa taarifa ya kazi za chama na
Serikali,kuzindua ukumbi wa mikutano wa Jimbo pamoja na kukabidhi
Vyarahani na Kompyuta kwa vijana wa jimbo la Mpendae.
Mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.Salim Hassan Abdullah Turky akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Amani,katika
jimbo la Mpendae mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Amani,katika jimbo la Mpendae
mapema leo asubuhi,ambapo pia alipokea taarifa taarifa ya kazi za chama
na Serikali,kuzindua ukumbi wa mikutano wa Jimbo pamoja na kukabidhi
Vyarahani na Kompyuta kwa vijana wa jimbo la Mpendae.
Mlezi wa mkoa wa Mjini Magharibi na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mara baada ya msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kuwasili mkoa wa Mjini Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua Ofisi ya Tawi la CCM Nyerere B,katika Wilaya ya Amani,ndani ya Jimbo la Magomeni Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipiga makofi mara baada ya kushiriki ujenzi na uzinduzi wa Ofisi ya tawi la CCM-Kilimahewa Juu,ambalo lilichomwa moto na kuvunjwa kabisa wakati wa harakati za kundi la Muamsho katika jimbo la Amani.PICHA NA MICHUZII JR-ZANZIBAR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...