Katibu
Mkuu Ndugu Kinana sambamba na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Ujumbe wake ukipokelewa na vijana wa CCM jimbo la
Donge wakiongozwa na Mbunge wao Mh.Sadifa Juma Khamis,mapema leo
alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM-Donge Mtambalike wilaya ya
Kaskazini B.Katibu Mkuu Ndugu Kinana yupo katika ziara ya Visiwa vya
Unguja na Pemba-Zanzibar akihimiza Uhai wa chama cha CCM na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010
Pichani
kulia ni Mbunge wa jimbo la Donge na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana
Taifa (UVCCM) ,Mh.Sadifa Juma Khamis akimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman Kinana pichani kati mara baada ya kuwasili katika jimbo hilo
Wilaya ya Kaskazini B,mkoa wa Kaskazini B Unguja kwa ziara ya siku
moja.Ndugu Kinana aliwasili katika ofisi za CCM Donge Mtambalike na kupokea
taarifa ya chama ya wilaya na utekelezaji wa Ilani,na pia alizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya.
Mtunza
fedha wa kikundi cha ushiriki cha akina Mama ,Saccos (kukopa na
kuweka),Bi Mwatime Juma Omar akitoa ufafanuzi mfupi kuhusiana na
ushirika huo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Makamu wa Pili wa Rais-Zanzibar,Balozi Seif
Ali Idd wakitazama shughuli mbalimbali za vijana wa Mafunzo ya Amali
katika fani ya ushonaji.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wananchi na wafuasi wa CCM,katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Maskani ya CCM Kizota,jimbo la Kitope,Ndugu Kinana aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kuipigia kura na Waipigie kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa kwa kuwa ina mambo mengi mazuri yenye faida kwa Wanzibari.
Mbunge
wa Jimbo la Donge na Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana Taifa
(UVCCM),Ndugu Sadifa Juma Khamis akiwahutubia wananchi na wafuasi wa
chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
Maskani ya CCM Kizota,jimbo la Kitope.
Baadhi
ya Wafuasi wa chama cha CCM,wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Maskani ya CCM
Kizota,jimbo la Kitope
Sehemu ya umati wa watu uliofika kwenye mkutano huo wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd mara baada ya mkutano wa hadhara
kumalizika,shoto nyuma ya Balozi ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye.
PICHA NA MICHUZI JR-MKOA WA KASKAZINI B-UNGUJA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
PICHA NA MICHUZI JR-MKOA WA KASKAZINI B-UNGUJA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...