Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama mkazi wa sheia ya
Mbuzini,Bi.Khadija Issa Kibwana mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika jimbo la Mfenesini,Mkoa wa Magharini.Katika ziara hiyo ambayo ni ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010,Ndugu Kinana leo ametembelea majimbo manne likiwemo la Bububu,Mfenesini,Dole na Mtoni.Katika ziara hiyo Ndugu Kinana pia ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la Spice Solution Farm,lililopo katika kijiji cha Mwakaje,wilaya ya Mfenisini,mkoa wa Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa madarasa katika skuli ya Kidichi,Wilaya ya Mfenesini mkoa wa Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani shoto na Waziri Kiongozi Mstaafu Mh.Shamsi Vuai Nahodha wakishriki katika ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bububu,katika wilaya ya Mfenisini mkoa wa Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipanda moja ya kiungo katika shamba la Spice Solution Farm lililopo Mwakaje,Wilaya ya Mfenesini mkoa wa Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiangalia viungo mbalimbali vilivyosagwa na kusindikwa tayari kwa kuuzwa kwa wateja.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Vijana wajasiliamali walioko katika shamba la viungo (spice Solution Farm),lililopo katika kijiji cha Mwakaje,Mfenisini,mkoa wa Magharibi.Ndugu Kinana amelitembelea shamba hilo na kujionea shughuli mbalimbali zifanywazo na vijana hao wapatao 2600.
PICHA NA MICHUZI JR-ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...