Wananchi
wa Tanga mjini wakimpa mkono wa kumuga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuwashukuru
Watanzania kwa kuichagua CCM na kuwashukuru kwa imani yao kwa kutambua
chama kinaweza kuongoza.
Wananchi wakiwa wamefurika
uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru
wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa
uliofanyika mwezi Desemba 2014.
Wananchi wakiwa wamefurika
uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru
wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa
uliofanyika mwezi Desemba 2014.
Baadhi ya Viongozi
waliohudhuria mkutano Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa
kushukuru wananchi kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za
Mitaa kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa
January Makamba,Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Abdalah Kigoda
na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mheshimiwa Mboni Mgaza.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Tanga,katika uwanja wa Tangamano jioni ya leo,baada ya aliyewahi Kugombea Ubunge Tanga Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA mnamo mwaka 2010,Kassim Omar Mbarak almaarufu Makubel,alipotangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,baada ya kuvutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza na wakazi wa Mji wa Tanga kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa mwenyekiti wa chama CUF-Pongwe,Bwa.Mbaraka Saad Mbaraka kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
Wakazi wa mji wa Tanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alizungumza nao kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.
PICHA NA MICHUZI JR-TANGA
Kijani ni Neema tupu Shati la Mbaraka Saada Mbaraka aliyetoka CUF kuingia CCM linang'ara sana, si mchezo!
ReplyDeleteJamaa Bonge la Mjanja ameshituka na kuhamia CCM!!!
Tanga ni Wajanja sana!
ReplyDeleteWamesha soma alama za Nyakati wakatambua kuwa Upinzani ni kukalia Kuti kavu, kila mmoja wanahamia CCM!!!
Vyama kama CHADEMA na CUF Uchaguzi huu 2015 havina chao Mkoani Tanga.
ReplyDeleteWapinzani waliwarubuni sana wana Tanga na sasa mwameshituka Uchaguzi mdogo CCM imekwapua 97% ya Kura!