Pichani
juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Baadhi ya
wakazi wa mji wa Kizimkazi waliofika katika uwanja
wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kumsikiliza.Ndugu Kinana
ambaye leo anaikamilisha
ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la
kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi majiko ya gesi kwa vikundi vya
akina mama wa Makunduchi yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la
Makunduchi,Mh.Samia Suluhu na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh
Haroun Ali Suleiman.
Ndugu
Kinana akishiriki kupandisha mabomba kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa
maji wa Kibuteni-Makunduchi unaosaidiwa na jumuiya ya Milele Zanzibar
Foundation.Pichani shoto ni Afisa Maji Mkoa wa Kusini Unguja,Bwana
Hafidhi Hassan Mwinyi,ambaye alisema kuwa lengo la Mradi huo ni
kuhuwisha,kuiimarisha na kuikuza miundombinu ya maji safi na salama ya
Makunduchi Kibuteni ili iweze kutoa huduma vizuri na kwa ubora
unaohitajika kwa walengwa wake.Mradi huo unakisiwa kugharimu kiasi cha
shilingi milioni 650 na ushehe.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na wanachama wengine,wakiwaongoza wanachama
wapya wapatao 518 kula kiapo mara baada ya kujiunga na chama hicho
sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Kizimkazi wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa
Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kwa minajili ya kumsikiliza
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya
siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa
chama na kukagua Utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...