Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal (wa kwanza kushoto) wakisikiliza hotuba ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati wa tarfija ya mwaka mpya aliyowaandalia wenza wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania tarehe 10.1.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Anna Mkapa wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nje hapa nchini.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAMA yajivunia mafanikio katika sekta ya elimu
Taasisi ya WAMA Foundation imefanikiwa kupanua fursa za elimu kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2014.
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete wakati Akiongea na wenza wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali katika ghafla fupi ya kuukaribisha mwaka mpya 2015 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam,
Mama Salma alisema kuwa baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi ya WAMA ni kukamilika kwa sekondari ya WAMA Sharaf katika Manispaa ya Lindi.
“Ninayo furaha kuwataarifu kwamba ujenzi wa shule ya sekondari ya WAMA Sharaf umekamilika, shule ambayo itaongeza idadi ya wasichana wanaofaidika na WAMA” Alisema Mama Salma.
Aidha, aliitaja Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama kuwa sehemu ya mafanikio ya Tasisi hiyo ambayo ina idadi ya wanafaunzi zaidi ya 400 na inatarajia kuchukua wanafunzi 90 mwaka 2015, ambao ni yatima na wanaotoka kwenye mazingira magumu.
Akiongelea kuhusu mafanikio mengine Mama Salma alisema ni pamoja na kuimarisha afya ya mama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo, kupunguza mimba za utotoni, na kupunguza kasi ya maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Mama Salma aliwashukuru wadau wote wanaofanya kazi kwa kushirikiana na WAMA wakiwemo Mashirika yasiyo ya Serikali kwa misaada na kuwaomba waendelee kushirikiana ili kutoa mabadiliko chanya katika jamii husika.

Aidha, kwa niaba ya wenza wa mabalozi waliohudhuria ghafla hiyo, Mke wa kiongozi wa mabalozi nchini Bi Celine Mpango alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa juhudi anazofanya katika kumkomboa mtoto wa kike na mwanamke kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...