Fainali za michezo mpira wa miguu kutafuta bingwa wa wilaya ya Mvomero zinazokwenda kwa jina la Makalla Cup zimehitimishwa jana kwa mamia ya watazamaji kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Kialawa, Kijiji cha Bwagala ambapo ulizikutanisha katika Fainali Timu ya Koloni ya Bwagala na timu ya Mkuyuni ya Mlali na hatimaye ubingwa wa Makalla Cup ulikwenda kwa Timu ya Koloni kwa kuifunga Mkuyuni mabao 2-1.

Mgeni rasmi na mdhamini wa Mashindano hayo ya Makalla Cup alikuwa Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla ambaye katika Hotuba yake alizipongeza timu zote 124 zilizoshiriki kuanzia ngazi ya Kata,Tarafa na hatimaye Wilaya.

Alisema lengo la michezo hiyo ya kihistoria ni kuendeleza vipaji, kuwaleta pamoja vijana bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.

kwa upande wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo,mshindi wa kwanza amejipatia fedha taslim shilingi milioni Moja na kombe kubwa la shilingi laki tano, mshindi wa pili alipata shilingi laki Sita na kombe la sh. laki tatu na mshindi wa tatu amepata shilingi laki Tano na kombe la shilingi laki mbili.

Mh. Makalla ameishukuru Benki ya BOA kwa kusaidia jezi seti 8, na pia ametoa shukrani zake kwa vyombo vya habari vyote,timu zote zilizoshiriki ,chama cha mpira wa miguu Mvomero,viongozi ngazi zote Mvomero na wananchi wa Mvomero kwa ushirikiano mkubwa waliompa kwa kufanikisha mashindano hayo makubwa na ya aina yake

Ameaidi kuendeleza michezo na akiwashukuru viongozi wa Kiwanda cha Mtibwa kwa kuhudhuria na kuibua vijana ambao watawasajili kwenye timu yao ya Mtibwa sugar
Mgeni rasmi na mdhamini wa Mashindano ya Makalla Cup,Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla  akikabidhi kombe na fedha shilingi milioni moja kwa Nahodha wa timu ya Koloni ya Bwagala ambao ndio mabingwa wa mashindano hayo.
Mgeni rasmi na mdhamini wa Mashindano ya Makalla Cup,Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla  akitoa hotuba yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...