Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Jamuhuri ya muungano Mhe.Bw.Seif Rashid na waziri wa afya wa ZanzibarMhe. Rashid Seif Suleiman, Siku ya jumapili 25 januari 2015 walikutana na kuongea na baadhi ya watanzania waishio nchini ujerumani katika hoteli ya Martim Hotel mjini Berlin.
 
Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na  balozi Tanzania nchini Ujerumani mheshimiwa Bw.Philip Malmo,katika mkutano huo mawaziri hao wote walielezea jinsi wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafakia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila Mtanzania atatanufaika na huduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao. 
 
Watanzania waishio ujerumani wamefarajika sana na mkutano huo,pia mawaziri wamewataka watanzania waishio ughaibuni  kuchangia kuwekezakatika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi ,mawaziri hao wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.
 Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa(katikati)makam mwenyekiti wa UTU Bw.Peter Kazaura(mwenye kitamba shingoni) mdau Shah wa jiji la Berlin Mwenye kofia nao walikuwapo

 Mkuu wa bendi ya Ngoma Africa Kamanda Ras Makunja akiwa Mhe.Philip Malmo Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ,katika mkutano katika hoteli ya Maritim mjini Berlin.
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii ambaye  pia ni mbunge wa Rufiji Mhe.Seif Rashidi akiwa na Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mjini Berlin,Ujerumani.
 Waziri wa Afya wa jamuhuri ya muungano mhe.Seif Rashidi akiongea na watanzania waishio Ujerumani,
 Waziri wa Afya wa Tanzania Mhe.Seif Rashid akiwa na baadhi ya watanzania nchini Ujerumani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Naona waziri yupo na watanzania wa ujerumani harafu kamanda Ras Makunja naona kajikoki kila kitu ukimchokoza tu virungu

    ReplyDelete
  2. eh! bwana saralehh kamanda ras makunja umependeza uko Berlin naona upo uraiani kama raia wengine

    ReplyDelete
  3. TWILA KAMBANGWAJanuary 26, 2015

    haya bi jokha na sele na waona full kujiachia, mjomba shah kumbe ulikuwepo nice, haya twambieni mlikuwa na hoja gani na mmekubaliana nn? maana mh amemuondoa mh Mwakyembe sehemu ambayo alikuwa anaiweza na anawaweza leo hii sijuwi kapelekwa wapi? mliileta hiyo hoja?

    ReplyDelete
  4. kamanda ras makunja akiwa katika vazi kiraia nje ya jukwaa katulia tena binadamu kweli kweli

    ReplyDelete
  5. weh Peter Kazaura huyo mliyemweka katu chui wa nguvu ukivuka anga zake anakujerui

    ReplyDelete
  6. Ras Makunja hiyo pete yako nikuvue nimefika bei

    ReplyDelete
  7. te !te! Kikamanda ketu ras makunja kilikuwepo kimependeza kweli uraiani

    ReplyDelete
  8. naona kamanda ras makunja umejinyonga si mchezo umependeza,una haja tena ya kuvaa gwanda

    ReplyDelete
  9. wewe ras makunja utaki kupiga konozz? kwa wadada au ndio umeuchuna unajifanya kipofu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...