Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ghalani katika mji mdogo wa Himo jimbo a Vunjo alipokuwa akiwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukipa ushindi chama chake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa ulimalizika hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza na wananchi katika jimbo la Vunjo,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuwashukuru kwa kuchagua wenyeviti wengi waliotokana na chama cha NCCR-Mageuzi,mkutano uliohutubiwa pia na Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ,Ndolakindo Kessy akizungumza katika  mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji.
Mmoja wa wakazi katika jimbo la Vunjo ,Elizabeth Mrema  akimkabidhi Mbunge wa kuteuliwa na rais ,Mh James Mbatia zawadi ya shati la Kitenge kwa niaba ya wakazi wa jimbo la Vunjo ,kuipeleka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu ,Joseph Waryoba.

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...