Kaka Michuzi,
thank you for your good work. Its always a proud moment seeing the good work you do in our social media circles. Keep up and God bless you.
My problem:
Am a young man looking for a suitable house to relocate to (plans of settling down are knocking). Given the housing situation in Dar I have met 'Dalalis' after 'Dalalis' going round looking for a house in  Tegeta, Mbweni,Boko,Ununio & Masiaya areas. 
I think it has to do with my budget. Tsh 250,000/= per month for a simple neat 2 bedroom self contained house in a gated compound (have a car so security is top on the list). Is that too small a figure?Its all I can manage. Jamani nimetafuta wacha masihara!
I think am a relatively wonderful tenant and my current landlord can write a recommendation on that if need be. Could you possibly post for me this ad so that anyone who stays around those areas or along bagamoyo road and has a suitable place that he/she would like a great tenant could contact me? a simple email or pictures of the place to this email will do.  tegetaescrow@yahoo.com . 
Thank you kaka Michuzi!!!!!......

PS:
5 years on you are still the first blog 
I check in the morning at work before my bosses come in!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Weka namba yako ya simu hapa watu tukupigie simu.

    ReplyDelete
  2. UKO SERIOUS , KUNDUCHI BEACH KUNA NYUMBA INAPANGISHWA usd 1,000 KWA MWEZI KAMA UKO TAYARI SEMA

    ReplyDelete
  3. Tsh 250000.00/mwezi vyumba viwili na geti kwa ajili ya usalama wa gari! Hupati.

    ReplyDelete
  4. wewe ndugu mtafuta nyumba, kweli wewe ni mtanzania halisi unaishi jijini Dar?.

    hizo pesa zako shs 250,000= tafuta chumba uswahilini.kama mbagala, tandale kwa kina diamond
    huku tegeta huwezi pata katu katu.

    kama una $ kuanzia 1000 njoo usaidiwe

    ReplyDelete
  5. email address yako tu, mie hoi!

    ReplyDelete
  6. Huwezi kupata nyumba yenye sifa unazotaka sehemu hizo kwa 250,000 kwa mwezi.

    ReplyDelete
  7. sio rahisi but miracles do happen

    ReplyDelete
  8. watu wana majibu......

    ReplyDelete
  9. Kwa hizo Pesa, Nenda Mbagala Au Manzese kwa mfugambwa. Huku Tegeta Tuachie sisi tuliobeba Pesa za viroba.

    ReplyDelete
  10. Aaahhh bw. Michuzi umeanza na mafumbo yako mi nimestuka na hiyo email yako unataka kutupima tu kwa hilo mi hunipati huna mawasilano mengine zaidi ya hiyo email.

    ReplyDelete
  11. Nyumba zipo nyingi tu...kuanzia 250,000/= mpaka nzuri kabisa kwa 450,000/= . Mimi ninaishi tegeta na ndio bei za huku. Acheni mambo yenu. Hiyo tegeta ya $ 1000/=ni Ipi?

    ReplyDelete
  12. Nina nyumba laki sita kwa mwezi. Hiyo 250,000 huwezi pata "nyumba" labda "chumba" uswazi.

    ReplyDelete
  13. Wabongo si ndio zao...wanaamua tu kutamka bei mtu anakuambia nina nyumba ya sh laki sita kwa mwezi...ukienda kuiona haina hata thamani hiyo.....ukimuuliza anakwambia maeneo haya ni ghali sana....au hata nyumba ile na ile bei ndo hiyo. Yaani watanzania mtu ana amua tu kupanga bei kichwani...na kutokana na shida mtu kuhangaika kutafuta nyumba anaamuwa Kukupa....dalali anaweza akamwambia mwenye nyumba kuwa nyumba yako hii unapangisha kwa sh 300,000/= mimi nitakutafutia mteja wa sh 500,000/= basi mtu anakubali....kiujumla biashara ya upangishaji kibongobongo haina utaratibu nimaamuzi tu ya mtu bila kuangalia uhalisia....mtu anaamua tu nyumba dola 1000/= au 2000/= coz eti ina tiles, aluminum na Ac. Au anakwambia huku tegeta bwana bei zake ndio hizi...mi nafikiri kuwe kuna wataalamu/na serikali kufuatilia uhalali kodi za pango/ kodi elekezi ya eneo husika/ ubora wa nyumba/wa kufanya mahesabu sahihi ya kodi halali ikiwemo VAT na kodi nyinginezo halali( mpango uwe kama tunavyonunua mafuta ya magari yetu au tu tunapolipa nauli kwenye mabasi kutokana na ubora wa basi pamoja na umbali) kiukweli hata sisi tuliobahatika kwenda nje ya Tanzania ukilinganisha gharama za kupanga nyumba utaona ni kubwa kuliko usahihi wake. Ki ujumla nimalizie kwa kusema ni biashara inayojiendesha bila sheria wala mipango ndani ya nchi yetu na inaumiza sana walalahoi kwa kipindi kirefu.

    ReplyDelete
  14. Anonymous 13, umenena. Kama unataka laki 6 or more kwa nyumba yako then swali la jamaa halikuhusu. Kakosa nini kuwa mkweli kulingana na hali yake! Tuwe waungwana kuliko kuporomosha kebehi zisizo na maana, au ndo madalali nyie! Nfyuuuuuuu!

    ReplyDelete
  15. Weka simu yako tukupigie but honestly bei hiyo na kiwango cha nyumba Tegeta kupata itakuwa miracle. Ninayo nyumba ila kwa 800,000/Mwezi. Very secure nakiwango cha juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...