Mflame Abdullah bin Abdul-Aziz wa Saudia (pichani) aliyefariki usiku wa kuamkia leo anatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Ijumaa. Taarifa iliyotangazwa na televisheni ya nchi hiyo imesema kuwa, uongozi umechukuliwa na Salman bin Abdulaziz ndugu wa Abdullah.
Mfalme huyo aliyekuwa anakaribia umri wa miaka 90 alipelekwa katika hospitali moja ya mjini Riyadh mwanzoni mwa mwezi huu kwa ajili ya matibabu baada ya hali yake ya kiafya kuzorota ambapo alikuwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji.
Habari zinasema kuwa, Mfalme Abdullah amefariki dunia saa saba za usiku wa kuamkia leo kwa majira ya Saudia. Ofisi ya ufalme ya nchi hiyo imetangaza kuwa, sala ya maiti itasaliwa baada ya sala ya alasiri ya leo katika chuo cha Imam Turki bin Abdullah mjini Riyadh.
Aidha habari zimeongeza kuwa, Salman bin Abdulaziz Aal Saud amepata baiya ya kuwa mfalme kwa mujibu wa katiba ya utawala wa Saudi Arabia ambapo naye amemteua Muqrin bin Abdul-Aziz, ndugu wa baba mmoja wa Mfalme Abdullah kuwa mrithi wa kiti cha ufalme baada yake.
Mfalme Abdullah aliyezaliwa mjini Riyadh, alikuwa mtoto wa 13 wa mfalme Abdul-Aziz, mwasisi wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo. Baadhi ya duru zinasema kuwa, bado kuna mivutano ya kuwania madaraka kati ya watu wa ukoo wa Aal Saud. Kupata chanzo BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...