Afisa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Chamwino Bw. Denis Vagela (kushoto)
akizungumza na Vijana wa kikundi cha Wajasiriamali wa Wilaya ya Chamwino
wanaojishughulisha na utengenezaji wa Sabuni za maji, Batiki na ufundi walipotembelewa kwa
ajili ya kuangalia mradi wao leo Mkoani Dodoma. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, na aliyekaa ni Afisa Vijana Wizara ya
Habari Vijana Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
Wakwanza mbele ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi Ester Riwa akiangalia mashine ya kukamua alizeti iliyotengenezwa na Vijana wa
kikundi cha Chachu ya Maendeleo Dodoma wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Mkoa wa
Dodoma. Kulia ni kijana wa kikundi hicho Bw. Ayoub Athumani.
Kijana Samwel Nagija kutoka kikundi cha vijana cha Chachu ya Maendeleo Dodoma
kinachojishughulisha na utengenezaji wa mashine za kusaga na kukoboa, mashine za
kutengeneza matofali, mashine za kukamua alizeti, na ujenzi wa vitanda na madawati ya chuma
akiendelea na ujenzi wa mashine ya kusaga leo Mkoani Dodoma.
BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...