Mashindano ya awali (Preliminary show)ya fainali za kumtafuta mrembo wa Miss Universe Kimataifa huko jijini Doral, Miami-Marekani yamefanyika jana tarehe 21 huku jumla ya warembo 88 kutoka nchi tofauti duniani wakipita na mavazi ya Kitaifa(National Costume), ufukweni(Swim Suit) na magauni ya usiku(Evening gown). 
Mrembo wa Tanzania, Nale Boniface (pichani)  ni mmoja wa washiriki wa mashindano hayo ambapo fainali zake zitahitimishwa jumapili, januari 25 huko Marekani. Siku chache zikiwa zimebakia kuhitimisha shindano hilo, washiriki wote walipata nafasi ya kuzungumza na kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya habari huku wakizungumzia mawazo yao kuhusu fainali hizo.
 Shindano hilo la awali liliendeshwa na mrembo wa Miss Universe 2013, Gabriela Isler and Roxanne Vargas. Shindano hili la awali lilikuwa na umuhimu kwa washiriki wote kwani ndipo wanapopatikana 16 bora ambapo watatangazwa siku ya fainali za shindano hilo jumapili ya tarehe 25.Shindano hili ni la 63 kufanyika toka kuanzishwa kwake. 
Mshiriki wa Tanzania katika shindano hili alivaa vazi lililobuniwa kutokana na zao la MKONGE. Mkonge ni zao linalostahmili ambapo linaweza kustawi katika hali ya ukame na nchi zenye uoto usio na rutuba. 
Zao hili pia lina magonjwa machache sana ambayo mara nyingi halihitaji dawa yoyote. Pia zao hili linasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupata unyevu wa anga. Zao hili linaweza kupandwa wakati wowote wa mwaka na kuvunwa kwa mwaka mzima. 
Zao hili pia haliathiriwi na moto,na ni mazao machache sana katika dunia hii yenye sifa kama hizi. Hivyo, vazi la mshiriki wetu wa Tanzania katika fainali za Miss Universe limebuniwa na kutengenezwa kutokana na zao la Mkonge.
Vazi la jioni
Vazi la taifa
Vazi la kuogelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Vazi la Taifa???

    ReplyDelete
  2. Vazi la Taifa gani? Jaribuni sana kuwa makini na mnachoandika, vinginevyo mnaleta aibu kwa Taifa. Hili sio vazi la Taifa la Tanzania!!!! Usituletee aibu!!!!

    ReplyDelete
  3. Salaaale! Jamani mtansameh, maana hiilo vazi la Taifa binafsi naliona limekaakaa na kutaka kufanana mithili ya mdudu kwetu huwa tunamwita 'Tandarusi', Au labda mngetufafanulia ni Taifa gani isiwe tunali criticize bure! Lakini kama ni Taifa letu la Tanzanzia, kuna haja ya kulifanyia 'review' au kama limekosekana basi hata 'Dera' lenye rangi ya bendera yetu, full heshima.

    ReplyDelete
  4. kumbe ndo vazi letu hilo?????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Vazi la taifa gani?

    ReplyDelete
  6. Mtakuwa mna matatizo kichwani nyie. Aliyewaambia hilo ni vazi la Taifa ni nani? Mnajitungia vinguo vyenu mnaviita vazi la Taifa. Serikali kwenye haya mashindano lazima muwe na mkono, mjue mtu anaenda kufanya nini na kama kuna category ya vazi la taifa awaonyeshe anaenda kuvaa nini...sio kuvaaa vitu vya ajabu na kusema ni vazi la Taifa.

    ReplyDelete
  7. Michuzi tuombeni radhi! hilo ndio vazi la Taifa la TAnzania au la kabila la huyo mwanamwari hapo?

    ReplyDelete
  8. kumbe vazi la Taifa kwa wenzetu kina mama tunalo tena zuri tuu..
    lakini hawataki kuvaa; jameni wanawake hawa...

    mdau; Tango Mike - Arusha

    ReplyDelete
  9. Vazi la ubunifu sio la taifa ila: Ni kutoka Taifa la Tanzania. Wote walivaa mavazi yao ya ubunifu kutoka mataifa yao labda ingewekwa hivyo ingelionekana vzr zaidi kuliko kulipua kuandika VAZI LA TAIFA. Hata kama ni la ubunifu, halipendezi limelipuliwa sana na design yake bomu. Inaelekea hawa wadada hawana bado watu wa kuwatengenezea mavazi mazuri ya ubunifu. Napita tu mmama mie.

    ReplyDelete
  10. Haya tena wa Bongo badala ya kumsifia Dada yetu mnashambulia mavazi lini Tutendelea????????

    ReplyDelete
  11. Kwanza kabisa Mh Mbunge wangu mtarajiwa haitaji kabisa kuomba radhi kwa yoyote yule wala vijana wake hawatakiwi kuomba radhi kabisaaa.

    Pili, Hacheni akili zenu ndogo za @^#^##^@ nani kawaambia amemaanisha ni vazi la Taifa, Ni kwamba kama akiwa mwakilishi wa mashindano hayo toka Tanzania bs ilo ndio vazi la kitaifa kutoka kwa mrembo huyo na mbunifu wake. Kuweni na akili za haraka haraka za kufikiria na sio kukimbilia kutoa maoni yasio na maana, zikiwekwa habari muhimu za kitaifa hamtoi maoni yenu ila zikija habari za namna hii na roho zenu mbaya za kwanini mnaanza kukurupuka na kuanza kuwaambia watu waombe radhi, Mnaijua radhi nyie ebu tulieni kidoooogo.

    ReplyDelete
  12. Hiyo bakora maana yake ni nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...