Mratibu
wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TNCHF), Camillius Haule (kulia)
akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano kati ya Maafisa wa NHIF na wadau
wao,juu ya Mpango wa Kikoa (Mutual Plan) unaoratibiwa na NHIF
uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msimbazi Center,Ilala
jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) Kanda ya Temeke,Ellentruda Mbogoro (wa pili kulia),Afisa
Uratibu wa NHIF kutoka Makao Makuu,Catherine Masingisa pamoja na Afisa Uratibu wa NHIF toka Temeke,Mbali Shitindi.
Afisa Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka Makao Makuu,Catherine Masingisa akitoa somo kwa wadau wa Mfuko huo kuhusu Mpango wa Kikoa (Mutual Plan) unaoratibiwa na NHIF uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau wa Mfuko huo,Sunagritha Mapunda akionyesha fomu alizokabidhiwa kwa ajili ya kujiunga na uanachama wa Mfuko huo.
Sehemu ya Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...