Na Frank Shija.WHVUM
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu inayojishughulisha na kazi ya kutafsiri Filamu
kwa Lugha ya Kishwahili Bw. Derick Mukandala maarufu kwa jina la Mzee Lufufu (pichani kulia) amekiri
kuwa kazi yake anaifanya kienyeji ili hali akifahamu ni makosa.
Kauli hiyo ameitoa leo katika kikao baina yake na Bodi ya Filamu ambapo alieleza kuwa
amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila kuzingatia utaratibu huku akijua kuwa ni
makosa kwa mtu kutumia kazi ya msanii mwingine bili idhini yake.
“Nikiri tu kwamba nimekuwa nikifanya makosa kwa kutafsiri Filamu bila kuwa na idhini ya
wahusika wa filamu hizo” Alisema Lufufu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...