Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea kutoka kwa Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Dkt. LU Youquing baadhi ya Vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa serikali ya China kwa ajili ya kusaidia shughuli za Bunge. Vifaa hivyo vyenye thamani ya Dola za Kimarekani laki moja vimekabidhiwia leo katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Spika jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza kutoa neno la shukrani mara baara ya kupokea vifaa hivyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Dkt. LU Youquing mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...