Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Haruna Lipumba (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo,alipofikishwa kujibu shitaka la kuhamasisha wanachama wa chama chake kufanya maandamano.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Haruna Lipumba akiwatuliza wanachama na wafuasi wa chama hicho kuacha kelele katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama na Wafuasi wa CUF wakiimba nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.Picha na Father Kidevu Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kweli Tanzania watu hawana kazi za kufanya. Hivi, uje kama huku nje ukute watu wanapoteza muda eti kuandamana kwa ajili ya siasa, atalipa nini bili ya maji, umeme, nyuma. Maana saa moja tu ni dollar. Yaani kweli maskini ni maskini tu na tajiri ni tajiri tu. Hongereni sana kwa maandamano na kucha shughuli zenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi sishangai kumuona mtu mwesi ulaya anaitwa kima. Na isitoshe mkipigwa risasi munaanza kulalamika because I am black. Halafu munaanza kuandamana. Sasa nyinyi huko ulaya hamna kazi na kwanini munaandamana?.

      Delete
    2. Mimi niko nje na nimeona maandamano mengi tu. Au nje Unamaanisha Somalia! !?!!?? Acha ufudutu nsugu

      Delete
  2. huko wapi kusikokua na maandamano?

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza hapo juu unadhani ''Haki Sawa Kwa Wote'' walionayo huko 'Nje' iwe Marekani au Ulaya waliipata hivi hivi bila kuitafuta?

    Jaribu kujiuliza mfano haki ya wanawake kupiga kura Uingereza waliipata wakiwa wamejikalia majumbani mwao au makazini mwao ? Au walipata kwa maandamano na harakati za kudai ''haki sawa kwa wanawake na wanaume'' ktk eneo hilo moja tu la upigaji kura!

    Soma historia usidhani demokrasia, haki za binadamu, mishahara inayokidhi wewe kulipa bili n,k waliletewa buree bila maandamano n.k

    Demokrasia,maji safi, huduma bora za afya, usafiri bora, elimu kwa wote pia huko nje waliipigania kwa namna nyingi ikiwemo maandamano, harakati n.k

    Hivyo usiwe mwepesi kuwabeza hao wanaoshinda ktk maandamano n.k wakitafuta ''Haki Sawa kwa Wote''

    Najua Michuzi pia utatoa nafasi kwa mawazo haya mbadala ktk kuona matukio mbalimbali nchi na nje ya nje kwa michango ya hoja iliyobeba mifano ya kihistoria.

    Mdau
    Diaspora

    ReplyDelete
  4. Wewe anon wa kwanza acha ujinga. Kuandamana ni haki ya raia kikatiba awe mfanyakazi au si mfanyakazi, ujinga wako unakufanya ushindwe kutofautisha kati ya kuandamana, umaskini na utajiri. Kuandamana ni freedom of speech and expression vitu ambavyo Tanzania vinakandamizwa.Maandamano ya umma yamewang'oa madikteta. Rudi shule ukasome uondokane na ujinga, elimu haina mwisho.

    ReplyDelete
  5. wewe mdau wa nne ni mjinga na hufai kuwa mwalimu kabisa, hata wanao unawaelekeza kwa matusi ili waelewe. Mbona wenzako wameeleza kwa lugha isiyo ya matusi? jifunze kufundisha waliokosea na sio kufundisha kwa kutukana. Nawe rudi shule ukajifunze namna ya kutoa majibu mazuri kwa waliokosa. Hapa ni uhuru wa kutoa maoni na sio uhuru wa kushindana kwa matusi. Mjinga kabisa wewe

    ReplyDelete
  6. mdau wa kwanza ambapo hakuna maandamano ni mbiguni tuu. Labda wewe ni moja ya malaika ulioko huko tunaomba baraka zako na sisi tuache kuandamana

    ReplyDelete
  7. We Anon wa kwanza hapo juu unachoelezea ni utumwa na umaskini walionao wavuja jasho kukosa hata muda wakujitafakari chochote, yes na kuandamana. Huko huko majuu, matajiri ndio wenye muda, waliobaki hawana tofauti na watu wa dunia ya tatu!!

    Na takwimu zinaonesha kwa miaka 30 au zaidi iliyopita wavuja jasho hawajanufaika na kukua kwa uchumi. Sana sana, ni kukopa na kufanya kazi zaidi ya moja ndio maana wanaonekana kana kwamba kuna unafuu!!

    Hapa kwetu acha watu watafute haki zao tusije tukaingia kwenye mifumo kama hiyo ya "majuu"!!

    ReplyDelete
  8. annoy wa kwanza huko kwenu kusikokuwa na maandamo si kila kitu mnapata..maji..umeme..barabara..kazi..ndo mana mko bize..sie huku hakuna vyote ndo mana tunaandamana..
    shwaini wahad...

    ReplyDelete
  9. Kweli Tanzania watu hawana kazi za kufanya. Hivi, uje kama huku nje ukute watu wanapoteza muda eti kuandamana kwa ajili ya siasa, atalipa nini bili ya maji, umeme, nyuma. Maana saa moja tu ni dollar. Yaani kweli maskini ni maskini tu na tajiri ni tajiri tu. Hongereni sana kwa maandamano na kucha shughuli zenu.
    Wewe anon wa kwanza acha ujinga. Kuandamana ni haki ya raia kikatiba awe mfanyakazi au si mfanyakazi, ujinga wako unakufanya ushindwe kutofautisha kati ya kuandamana, umaskini na utajiri. Kuandamana ni freedom of speech and expression vitu ambavyo Tanzania vinakandamizwa.Maandamano ya umma yamewang'oa madikteta. Rudi shule ukasome uondokane na ujinga, elimu haina mwisho.
    wewe mdau wa nne ni mjinga na hufai kuwa mwalimu kabisa, hata wanao unawaelekeza kwa matusi ili waelewe. Mbona wenzako wameeleza kwa lugha isiyo ya matusi? jifunze kufundisha waliokosea na sio kufundisha kwa kutukana. Nawe rudi shule ukajifunze namna ya kutoa majibu mazuri kwa waliokosa. Hapa ni uhuru wa kutoa maoni na sio uhuru wa kushindana kwa matusi. Mjinga kabisa wewe
    We Anon wa kwanza hapo juu unachoelezea ni utumwa na umaskini walionao wavuja jasho kukosa hata muda wakujitafakari chochote, yes na kuandamana. Huko huko majuu, matajiri ndio wenye muda, waliobaki hawana tofauti na watu wa dunia ya tatu!!

    Na takwimu zinaonesha kwa miaka 30 au zaidi iliyopita wavuja jasho hawajanufaika na kukua kwa uchumi. Sana sana, ni kukopa na kufanya kazi zaidi ya moja ndio maana wanaonekana kana kwamba kuna unafuu!!

    Hapa kwetu acha watu watafute haki zao tusije tukaingia kwenye mifumo kama hiyo ya "majuu"!!


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...