Kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Sudan,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa MArk Mwandosya alipata nafasi ya kuwa na mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Sudan,Mheshimiwa Ali Osman Mohammed Taha;kutembelea nyumba ya makumbusho ya Sudan;na kutembelea jengo la kumbukumbu la shujaa wa Sudan,al Mahdi.
Waziri Mwandosya,kushoto,akimkabidhi Mheshimiwa Ali Osman Mohammed Taha,Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu,zawadi ya kinyago kutoka Tanzania.
Walio mstari wa mbele kuanzia kushoto ni:Wallace Chiwawa kutoka Mamlaka ya Usalama wa Usafiri wa Anga Tanzania,TCAA; Ikhlass Abdellatief, Mkuu(Chief Curator) wa Nyumba ya Makumbusho Sudan;Waziri Mwandosya; Mama Lucy Mwandosya;na Ngusa Izengo, Katibu wa Waziri.
Nyuma yao kutoka kushoto ni: Ndugu Felix Ngamlagosi, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA; Mhandisi Clemence Kichao kutoka TCRA; Abd El Aziz el Obaid,Afisa Itifaki wa Sudan; Mama Grace Nsanya wa Wizara ya Maji;na Ndugu David Mziray kutoka SUMATRA. Jumba la Makumbusho lilijengwa kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa chini ya uratibu wa UNESCO ili kutunza malikale zilizookolewa wakati wa ujenzi wa Bwawa la Aswan High na ambalo lilizamisha eneo kubwa kaskazini Sudan.
Waziri Mwandosya akitoa heshima kwenye kaburi la shujaa wa Sudan na kiongozi wa dini Muhammed Ahmad al Mahdi, na jenerali aliyewashinda waingereza,waturuki,na wamisri huko el Obeid mwaka 1883 na Omdurman mwaka 1885.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...