Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Sudan jana amtembelea moja ya miradi mikubwa ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabwawa ambao unaendeshwa na Kampuni ya Merowe Dam Electricity Company.
Mradi huu ambao uko Kaskazini mwa Nchi ya Sudan umejengwa kwa gharama ya USD 2.0 milioni ambapo Serikali ya Sudan imechangia 30% na zilizobaki ilikuwa misaada na mikopo kutoka kwa wafadhili
Mradi umejengwa kando kando ya Mto Nile na una uwezo wa kuzalisha 1,250 megawati unachangia 60% hadi 70% ya mahitaji ya nishati ya umeme nchini Sudan. Mkurugenzi Mkuu wa Merowe Dam Electricity Company, Bw. Mahgoub Eisa Khalil amemtembeza Waziri na Ujumbe wake sehemu mbalimbali za mradi kama inavyoonekana katika picha zifuatazo:
.jpg)
Prof. Mwandosya, (wa pili mbele) ,na ujumbe wake, wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Ashraf Mustafa,kuhusu usimamizi,udhibiti,na uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha umeme.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ( wa sita toka kushoto) na ujumbe wake wakiwa na Uongozi wa Bwawa la Umeme la Merowe wakiwa mbele ya Kitoleo cha Maji(Spillway) Wengine kutoka kushoto ni: Ngusa Izengo,Katibu wa Waziri;David Mziray kutoka Sumatra;Grace Nsanya;kutoka Wizara ya Maji;Wallace Chiwawa,TCAA;Hassan Amin Mohammed Ahmed Omer,Mkurugenzi wa Usalama wa Bwawa;Ashraf Mustafa,Meneja wa Uendeshaji;Mahgoub Eisa Khalil,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Umeme,Merowe;Felix Ngamlagosi,Mkurugenzi Mkuu,EWURA;Mhandisi Mustafa Hussein,Afisa Mwandamizi,Wizara ya Maji na Umeme,Sudan;Meneja wa Kituo; na Clemence Kichao kutoka TCRA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...