Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikila watu wanne (4) raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kuwa na kibali

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema watu hao wamekamatwa tarehe 26/01/2015 majira ya 15:55hrs katika eneo la Nala kwenye Mzani wa Magari (Weight Bridge) Kata ya Nala Tarafa ya Zuzu Manispaa ya Dodoma wakiwa kwenye basi la Prince Munaa lenye namba za usajili T. 788 CNK likitokea Mwanza Kuelekea Dar es Salaam.

Kamanda MISIME amewataja watu hao kuwa ni:-

1.    SULYAN S/O JEYLAN mwenye miaka 23, Mkazi wa Kolobi – Ethiopia.
2.    KIAR S/O TAHIR HUSSEN mwenye miaka 25, Mkazi wa Agerifa – Ethiopia.
3.    BELAYNEH S/O DANIEL LEMENGO mwenye miaka 22, Mkazi wa Durame – Ethiopia.
4.    GALASA S/O AHMED GELIL mwenye miaka 24, Mkazi wa Robe – Ethiopia wakiwa na hati za kusafiria (Passport) zilizogongwa muhuri wa mwisho mpakani mwa Ethiopia na Kenya eneo la Moyale Border tarehe 16/01/2015.

Pia Kamanda MISIME amesema katika tukio hilo amekamatwa wakala anayehusika na kuwasafirisha watu hao aliyefahamika kwa jina la SULTAN S/O SAID RAMADHANI @ KUSHARUNGA mwenye miaka 31, mkazi wa mtaa wa Mecco Jijini Mwanza ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Kusharunga Tarafa ya Kimani Wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Wahamiaji hao walikuwa wanasafirishwa na wakala huyo kuelekea Afrika ya Kusini kupitia Mtwara – Msumbiji hatimaye kufikia Afrika ya Kusini. Aidha watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...