DSC_0300
Mratibu wa kituo cha TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).

Na Mwandishi wetu, Tarime-Mara
SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.

Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.

Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.

“Hii sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
DSC_0480
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (wa pili kushoto) akiwasili kwenye mahafali hayo pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...