Na Mdau Sixmund J.B
Shirikisho la mchezo wa Bao nchini (SHIMBATA) nilatarajia kufanya Tamasha kubwa la mchezo huo kwa
ajili ya kumuunze aliekuwa mlezi wa mchezo huo hapa nchini Hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawa
kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka mitano ntangu afariki Dunia.
Tamasha hili ambalo litaudhuriwa na wanafamilia ya Mzee Kawawa wakiwemo watoto wake Mh Vita R.
Kawawa Mbunge wa Namtumbo (CCM) na Mh Zainabu R. Kawawa Mbunge viti maalumu (CCM)
linatarajiwa kufanyika hapo kesho Tarehe 3/01/2015 katika viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM.
“Tamasha hili ni kubwa na nimahususi kwa kumuenzi Mzee wetu Mlezi wetu ambae pia ni Muhasisi wa
Taifa hili Mzee Kawawa, kwani mchango wake kwa maendeleo ya mchezo huu ni mkubwa sana, na pia
Mjane wa Hayati Mzee Kwawa atakuja kuungana nasi, yeye atakuja mchana saa sita hadi saa nane.
Nichukuwe nafasi hii kuwaalika watanzania wote, wanahabari na wafadhili mbali mbali wajitokeze
kuupa heshma mchezo huu kama sehemu ya kumuenzi Mzee wetu Kawawa”. Alisema Rais wa Bao
nchini Bw Mandei Likwepa.
Mchezo wa Bao ni moja ya michezo mikongwe hapa nchini na ambao unahistoria kubwa hasa katika
ukombozi wa Taifa hili la Tanzania, na umekuwa ukichezwa sana na Hayati Baba wa Taifa Mwl
J.K.Nyerere enzi za uhai wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...