Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam wakati alipozungumzia maandalizi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura, kura ya maoni ya Katiba mpya na uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu, kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Julius Mh.Julius Mallaba.
Baadhi ya waadishi wa habari wakiwa katika kutano huo.
NA CHALILA KIBUDA ,GLOBU YA JAMII DAR
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia Bilioni
293 kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mwaka huu
ikiwa ni lengo kukuza demokrasia nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar
es Salaam leo ,Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema
wamejipanga kuhakisha watu wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha ili waweze
kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa
pamoja na kupiga kura ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Lubuva alisema kuwa suala la kuwepo wanajeshi katika
uchaguzi , wataangalia jinsi gani ya
kufanya na kazi ya ulinzi ibaki
mikononi mwa jeshi la polisi.
‘’Suala la ulinzi wa jeshi
tuliweke na kuangalia jinsi gani tutafanya katika kuhakikisha wananchi
wanapiga kura kwa amani na usalama wa mali bila kuwa na hofu ya watu
wanaowalinda’’alisema Jaji Mstaafu
Damian Lubuva.
Aidha alisema uandikishaji wa majaribio, utambuzi wa alama
ya mpiga kura kwa kifaa cha BVR ulikwenda vizuri na mapungufu yaliyojitokeza
wataendelea kuboresha ili kila mtanzania aweze kujiandikisha na kupiga kura.
Alisema uandikishaji wa kanda ya kwanza utaanza Februari 16
hadi Machi 15 ambapo hakutaja mikoa gani itaanza hivyo wanaandaa orodha ya
mikoa na kanda katika jinsi ambavyo daftari la kudumu la mpiga litavyoweza kupita kuandikisha.
‘’Mambo yote yatakwenda sawa baada kukamilika kwa daftari la
mpiga kura likiwemo upigaji kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa na maoni ya wadau yataendelea kupokelewa
katika ofisi yetu’’alisema Jaji Lubuva
Tunaomba na sisi tulio nje ya nchi turuhusiwe kujiandikisha kupitia Balozi za nchi yetu.Hoja hii inaenda samba samba na jinsi tulivyoona wakati wa kupiga kura kwa wajumbe wa Bunge la katiba waliokuwa nje ya nchi.
ReplyDeleteHoja yako tutaifanyia kazi
ReplyDelete