Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini. Kutoka kulia ni  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mhe Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD). 
Nyuma yao ni mjane wa marehemu John Garang aliyekuwa Mwenyekiti wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng de Mabior na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Thobias Makoba. Meza kuu toka kushoto  wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wwa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol

baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE,

PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRMAN OF CHAMA CHA MAPINDUZI DURING THE SIGNING CEREMONY OF THE AGREEMENT ON THE RE-UNIFICATION OF SPLM OF SOUTH SUDAN, ARUSHA,
21ST JANUARY, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tuwatakie her njema watu wa South Sudan wapatane amani irudi ili wajenge nchi yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...