Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Christopher Ryoba Kangoye akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za maisha na ujuzi jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa Dodoma.
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada ya Uongozi kwa vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa wakifuatilia mada zilizokua zikitolewa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...