Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii Dar

Viongozi wa dini za kiislaam na kikristo wamesema dini ni za unyenyekevu na sio za kufanya maovu,ikitokea mtu mmoja katika imani anafanya maovu ni lazima akemewe ndani ya imani yake kwanza.

Wameyasema hayo leo katika kongamano la kujadili madhara ya misimamo mikali ya imani za kidini (Tafkiri) katika jamii na taifa lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo Katibu wa Taasisi za Kiislaam Wanazuoni,Sheikh Khamis Mataka amesema mambo yanayoendelea Afrika Magharibi na duniani kote wanatumia kufanya maovu kwa kutumia mgongo wa dini wakati maandiko ya mungu hayasemi hayo

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhary Islamic Foundation,Sheikh Khalifa Khamis amesema sasa umefika wakati wa kukemea maovu kwa wanaotumia mgongo wa dini kufanya hivyo.

Kwa upande wa Askofu wa Kanisa la EGS,Dk.Phirbert Mbepela amesema amejifunza kitu kwa dini ya kiislaam kuwa unataka watu wawe wanyenyekevu.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka akizungumza wakati wa kufungua kongamano la viongozi wa dini,lililofanyika kwenye ukumbiwa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhary Islamic Foundation,Sheikh Khalifa Khamis akifafanua jambo wakati wa kongamano la viongozi wa dini,lililofanyika kwenye ukumbiwa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.

Askofu wa Kanisa la EGS,Dkt. Philbert Mbepela akichangia mada kwenye kongamano la viongozi wa dini,lililofanyika kwenye ukumbiwa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Washiriki wa Kongamanp hilo wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. alyeanadika hili toleo inaonekana ametafasiri toka Swahili kwenda English kutumia google. kuna mchanganyiko wa Kiswahili na kiingereza ambacho hakijanyooka hata kidogo. Pia ahsante sana kwa kutupa taarifa vitu vinaeleweka.

    ReplyDelete
  2. Ahsante kwa kutupa taarifa za wanaharakati khalifa khamis na khamis mataka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...