Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Didas Mwilawi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha akisalimiana na Mwenyekiti wa wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya DAWASA Christine Kilindu alipowasili eneo zinapojengwa ofisi za mradi wa bomba kuu la maji kutoka Ruvu Juu zilizopo Kibaha.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiwa wameanza ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiangalia maungio ya mradi wa bomba jipya kutoka mtambo wa Ruvu Chini yaliyopo eneo la Mpiji wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...