Hii ilikuwa ni picha ya pamoja ya wasanii na mashabiki waliojitokeza kuunga mkono tamasha hilo la bure ambalo lina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika maamuzi yenye mustakabali wa nchi.

WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya aina yake pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Wakiongowa na  Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili, wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu hiyo.
Akizungumza kabla ya kuimba nyimbo zake kali,Mwana FA akitumia tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuchagua viongozi wanaowataka.
“Vijana wenzangu.., tusisubili watu wengine watufanyie maamuzi.., ni sisi wenyewe tunatakiwa kuamua tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema Mwana FA.
Mara baada ya kusema hayo, alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa sasa ukiwemo, mfalme ambao uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani hapo.
Mbali nma Mwana FA, pia Niki wa pili alipata mapoekzi makubwa viwanani hapo kwa nyimbo zake kali huku pia akisisitiza vijana kuchakua maamuzi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Wanamuziki wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni pamoja na Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and kenzo, Dogo Janja, Madee, Chegge, Temba, mwasiti na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya mashabiki waliojitokeza kuimba nao sambamba.
Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na Morogoro ambapo linalengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba mwaka huu.
Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro. 
 Mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk' akichana mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
 Baadhi ya wakazi wa Temeke waliojitokeza kwenye onesho hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar hapo jana.

Wasanii Chegge na Temba kutoka TMK Wanaume Family wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...