Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bei mpya ya king’amuzi kitakakochouzwa kwa shilingi 4000 sambamba na kifurushi kipya cha NYOTA cha malipo ya 4000 kwa mwezi, kulia pamoja naye ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Jacky Yu. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu.
Baadhi ya wateja waliokuwepo kwenye uzinduzi wa bei mpya ya king’amuzi kitakakochouzwa kwa shilingi 4000 sambamba na kifurushi kipya cha NYOTA cha malipo ya 4000 kwa mwezi. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka la kampuni hiyo lililopo ofisi za TBC1, Mikocheni-Bamaga jijini Dar es Salaam.

Kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali, StarTimes imekuja na kifurushi kipya na bei mpya ya king’amuzi kwa shilingi 4000/- tu gharama ambayo ni ya chini kabisa kutowahi kutokea nchini.

Akizungumzia juu ya huduma hii mpya Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Star Media Tanzania ambao ni wauzaji wa ving’amuzi vya StarTimes nchini, Bw. Jacky Yu amebainisha kuwa uzinduzi huu ni sehemu ya kutimiza ahadi kwa watanzania kwamba watakuwa wakitoa huduma bora na kwa bei nafuu ambayo kila mtu ataweza kuimudu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...