Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wametakiwa kuchangamkia promosheni ya Jaymillions ambayo ilizinduliwa juzi ili waweze kujishindia mamilioni ya fedha kwa kuwa droo ya kwanza iliyofanyika leo/jana mshindi wa milioni 100/- hakupatikana wakiwemo washindi kumi wa milioni 10/- na washindi mia moja wa shilingi milioni 1/-.

Mkuu  wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa  alisema leo baada ya kumalizika droo ya kwanza:“Natoa wito kwa wateja wetu kuangalia namba zao kama zimeshinda kila siku kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza  nafasi za ushindi kwa siku. 

Vodacom  itatoa mshindi mmoja wa Sh.100m/- kila siku, washindi kumi wa Sh.10m/- kila siku na washindi miamoja wa Sh.1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- hivyo nawasihi wateja wetu kuchangamkia hii fursa muhimu”.Alisema.

Twissa  aliongeza kusema kuwa  mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.

Alisisitiza kuwa  kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii na aliwahimiza wateja kuhakikisha wameangalia kila siku kama namba zao zimeshinda  ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kama ilivyotokea leo katika droo ya kwanza kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku.

Alimalizia kwa kusema kuwa promosheni hii  inathibitisha dhamira ya  kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom  na kuwataka kushiriki kwa wingi.

Katika droo ya leo washindi wapatao 116 wameweza kujishindia muda wa maongezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...