Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimuapisha Afisa
wa Jeshi la Magereza, Elmas Linus Mgimwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya
Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na
Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam leo. Kulia kwa Waziri Chikawe ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Pereira Ame Silima, na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa hati
ya kiapo Afisa Utumishi wa wizara hiyo, Ernest Maalugu kuwa Mjumbe wa
Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala
ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara
hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia-meza kuu)
akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia
masuala ya kiutumishi na kiutendaji wa askari katika Majeshi hayo, katika
Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...