Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (Kulia) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akifafanua jamabo kuhusu masuala ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Waziri wa Nchi aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (kushoto ) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam.
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (mwenye shati) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akiwaeleza wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) kuendelea kutoa ushirikiano wa kutekeleza majukumu ya ofisi hiyo, kwa Waziri mpya wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (katikati) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam (anayeandika) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli .
Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. William Lukuvi (Mb) ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi ambaye wakati wa kumkabidhi Ofisi aliyeshisha wadhifa huo wa Waziri Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akimhakikishia ushirikiano Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (kushoto ), wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam, (kulia ) ni Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (Kulia) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mmepewa nyazifa mpya, fanyeni kazi kwa bidii kuwasaidia wananchi na sio kulisha matumbo yenu na tamaa za rushwa na kupenda pesa. Mwogopeni Mungu na watumikieni wananchi kwa moyo usio na tamaa. Tanzania bila rushwa inawezekana. Makazi ya watanzania wengi yako duni sana sana imarisheni makazi ya watanzania ili kuondokana na kuishi maisha ya kimaskini.

    ReplyDelete
  2. Tanzania tunachekesha sana. Eti Naibu katibu mkuu akimhakikishia ushirikiano???? Mnatakiwa kuwajibika na mfanye kazi professionally siyo kuongelea mambo ya ushirikiano......ushirikiano wa nini mnatakiwa mheshimu sheria za kazi na mfanye kwa ukamilifu na nidhamu ya hali ya juu na wala kusukumwa......Mnachoambiwa mnatakiwa msikipuuze.

    ReplyDelete
  3. Utamaduni wa rushwa umeshajengeka Tanzania. Utamaduni ukishajengeka, ni vigumu sana kuuondoa. Sasa hivi Tanzania tunahitaji mapinduzi. Tunahitaji kiongozi mwanamapinduzi kama Chairman Mao wa China. Vinginevyo rushwa itaendelea. Hata wewe ndugu msomaji, kwa mfumo uliopo sasa hivi, kama ukipewa nafasi, Utakula rushwa. Kwa maana kama ukijifanya mwema ukaacha, mwingine atakula.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...