Kwa mwaliko wa Mheshimiwa Murtaz Musa Aballa Salim,Waziri wa Maji na Umeme wa Jamhuri ya Sudan,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ametembelea mradi wa ujenzi wa mabwawa katika mito ya Setit na Upper Atbara,jimbo la Gadaref na jimbo la Kassala nchini Sudan.
Mabwawa haya mawili yanaunganishwa na tuta moja lenye urefu wa km 13. Utakapokamilika Januari 2016 mradi huu utazalisha MW 320 za umeme na maji yatatumika pia kwa kilimo cha umwagiliaji na kuupatia maji mji wa Gadaref.
.jpg)
.jpg)
Waziri
Mwandosya,wa 4 kushoto akiwa mble ya kitolo cha maji (spillway) cha bwawa la
mto Setit.Wengine katika picha kutoka kushoto ni: Ngusa Izengo,Katibu wa
Waziri; Grace Nsanya,Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji;Mhandisi Mustafa
Hussein,Mshauri wa Ujenzi wa Mabwawa Sudan; Abd El Aziz El Obaid, Afisa
Uhusiano,Wizara ya Maji na Umeme,Sudan; na Mama Lucy Mwandosya.
Ujenzi
unaoendelea wa mfumo wa kupeleka maji kwenye mashine za umeme
( penstocks )
kwenye mto Upper Atbara
Waziri
Mwandosya,kulia,katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Hasabu Mohamed Abd El
Rahman,Makamu wa Rais wa Sudan ( aliyeshika fimbo) ,na Mheshimiwa
Murtaz Musa Abdalla Salim,Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan baada ya sherehe za
kuzindua kuanza kujaza maji kwenye mabwawa ya Setit na Upper Atbara,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...