Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.
Wakazi wa kijiji cha Ndoleleji wilayani Kishapu wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Profesa Muhongo ameahidi kuwapatia umeme kabla ya tarehe 30 Aprili, mwaka huu.
Wakazi wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo.
Wakazi wa Kata ya Seke Ididi wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu wakimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa tatu kutoka kulia) zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...