Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kushoto akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng. Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
Kijana Daudi Essau Seme kutoka katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited kushoto akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembelea mradi wa kikundi hicho wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...