Kama ilivyo kawaida
ya watu wa maeneo mengi hapa nchini,kwamba likitokea la kutoka basi huwa
ni faida kwa watu wengine.Mchana wa leo katika Makutano ya barabara ya
Nyerere rodi na Kawawa rodi,gari ndogo aina ya Toyota Hilux iliyokuwa
imebeba Vioo ilipatwa na mkasa na kupelekea mzigo wa vioo hivyo kuanguka
katikati ya barabara na kupasuka,hali iliyowapelekea vijana wanaofanya
biashara za mikononi (maarufu wa machinga) katika eneo hilo kuingia
barabarani na kuanza kujibebea mabaki ya vioo hivyo kama ionekanavyo
pichani hapa.hali iliyopelekea magari mengine yaliyokuwa yakiitumia
njia hiyo kuwakwepa vijana hao ili waendelee na kazi yao ya kujisevia vioo.

Hali hiyo ilidumu kwa muda kidogo na kupelekea Askari wa usalama barabarani kuyaongoza magari kupita pembezoni mwa barabara hiyo ili kuwaacha vijana hao ambao hawakutana kusikia la muadhini wala la mnadi swala.
Kazi ikiendelea.
yote hiyo ni njaa tu. Basi hiyo ndo Tanzania yetu, watu wote hawawezi kua na ajira sawa. Wengine ndo wanajiajiri kama hivyo waonekanavyo. Kila jema wapendwa
ReplyDeletehata kama vijana hao wasingekuepo bado magari yangeongozwa hivyo hivyo. tena itakuwa wamesaidia madereva wasiingie kukanyaga vioo hivyo
ReplyDeleteYote hii ni "NZALA"
ReplyDelete