Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imekabidhi simu za mkononi kama kitendea kazi kwa
walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya
Airtel Money vyenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara
wajasiriamali na kuwa mawakala wa huduma ya Airtel Money na kutoa
huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo
vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Simu hizo zilibabidhiwa kwenye muendelezo wa mafunzo yao ya
ujasiriamali yanayofanyika katika ukumbu wa Machinga Complex .
Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa masoko wa Airtel
Tanzania Haruna Ndyanabo alisema, “Airtel imeendelea kutoa mchango kwa
jamii kwa kuhakikisha walemavu hao wanafikia ndoto zao, kwa kuendelea
kuwapatia mafunzo mbali mbali ili kuhakikisha wanakuwa wafanyabiashara
madhubuti na tunaamini msaada wetu utasaidia kuboresha maisha yao kwa
kuwaongezea uwezo wakujiongezea kipato”.
“Kwani watu wanaoishi na ulemavu wanakabiliana na hali ngumu ya uchumi
kuliko makundi mengine katika jamii” ukizingatia kwamba ulemavu siyo
kigezo chakutoweza kufanya kazi.
Aliongeza kwa kusema “Shabaha ya kampuni ya Airtel hapa nchini sio tu
biashara bali pia kuona maisha ya jamii zinazotuzunguka yananufaika
na uwepo wetu kazi inayofanywa kupitia mfuko wa jamii wa Airtel na
ndio maana tupo mstari wa mbele katika kusaidia nyanda tofauti hapa
nchini.
Simu hizo zilikabidhiwa mbele ya mwenyekiti wa Taasisi ya haki za
binadamu na maendeleo ya kiuchumi bw. Abubakar Rakesh.
Mwenyekiti huyo alisema,” tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu
wakiwezeshwa ili kuweza kukidhi mahitaji yao na kuongeza kipato chao.
Tutaendelea kuwashukuru Airtel kwa misaada yao endelevu na kwa
kukiwezesha kikundi hiki kuweza kujiendeleza. Wito wangu kwa wanachama
wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka jitihada katika kazi zao
ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara zao.”
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (wa pili Kulia) akimkabidhi Rukia
Salum (wapili Kushoto) mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa
vibanda vya kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato na kuendeleza Maisha
yao ya kila siku. Wakishuhudia ni baadhi ya walemavu wengine waliowezeshwa na Airtel
katika mtaji huo.
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (kushoto) akimkabidhi Peter
Gwikama mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya
kisasa vya Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.
Afisa masoko wa Airtel Haruna Ndyanabo (Kulia) akimkabidhi Josephine John
mmoja kati ya walemavu waliowezeshwa na Airtel kwa kupatiwa vibanda vya kisasa vya
Airtel Money ili kuweza kijipatia kipato.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...