
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh, Wilman Kapenjama akikabidi funguo ya gari kwa Mshindi wa Promosheni Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika (60) ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni toka kushoto nyuma ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu, Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita, na Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva.

Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva (wakwanza kulia) akimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Anaefuata ni Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita na Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mkoani humo kwenye viwanja vya mashujaa mwishoni mwa wiki.

Meneja uhusiano wa Airtel bw, Jackson Mmbando akiongoza umati wa wakazi wa mkoani mtwara waliojitokeza katika viwanja vya Mashujaa kushudia hafla ya makabidhiano ya gari Toyota IST kwa mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel yatosha Mzee Sefu Namtapika mwishoni mwa wiki hii.

Mshindi wa gari aina ya Toyota IST mzee Sefu Namtapika akipongezwa na mke wake Bi… mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari alilojishindia kupitia promosheni ya Airtel Yatosha zaidi. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani mtwara mwishoni na wiki na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini mh, Wilman Kapenjama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...