.jpg)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (pichani) kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha,
anayesimamia Menejimenti ya Fedha za Umma (Public Finance Management).
Kabla
ya uteuzi wake, Dkt. Mwinyimvua alikuwa Msaidizi wa Rais wa muda mrefu wa
masuala ya uchumi.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue leo,
Jumatatu, Februari 2, 2015, imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwinyimvua ulianza
Jumamosi, Januari 24, 2015.
Dkt.
Hamisi Hassan Mwinyimvua ni mwanataaluma mwenye ujuzi na uzoefu mkubwa katika
uchumi.
Anayo
shahada ya kwanza ya B.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(1986), Shahada ya Uzamili ya M.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (1988) na Shahada ya Uzamivu ya PhD
ya uchumi kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Lund cha Sweden.
Dkt.
Mwinyimvua amekuwa mhadhiri wa miaka mingi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
ambako amepanda daraja kutoka Tutorial
Assistant, mwaka 1986-1988, Mhadhiri Msaidizi, mwaka 1988-1996, Mhadhiri,
mwaka 1996-2005, Mhadhiri Mwandamizi, mwaka 2005-2006 na Mkuu wa Idara ya
Uchumi ya chuo hicho mwaka 2006.
Dkt.
Mwinyimvua aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi, mwaka 2006, nafasi ambayo
ameishikilia hadi mwaka huu, 2015.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
2 Februari, 2015
Hongera sana Dkt. Mwinyimvua, MUNGU akubariki sana na akuwezesha katika kazi hiyo mpya. Mdau U.S.A.
ReplyDelete