Na Sylvester Onesmo wa 
Jeshi la Polisi Dodoma. 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kama Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa jana tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi Askari huyo. Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua Askari. 
 Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. 
 Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua. 
 Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi. 
Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu akiongoza leo waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Askari  Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI aliyeuwawa huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI SIRIL MALYA.
Wasifu wa marehemu ukisomwa 
Maombolezo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...