Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (kulia).
Mzee Augustino Mtauka akisaini fomu za usajili wa kituo
kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka
alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati),
usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally
Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF-Real Madrid
Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana
waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real
Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
Mtoto Osama Rashid akijaza fomu maalum kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Kulia ni mama yake Tatu Ali akishuhudia. Taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...