Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mke wa Msanii mkongwe wa muziki wa dansi na Mjumbe wa Bodi ya BASATA Bw. John Kitime kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa kuamkia Ijumaa ya Tarehe 13/02/2014.
Aidha, BASATA linatoa salamu rambirambi kwa kifo cha Baba Mzazi wa Msanii Dully Sykes, Mzee Abby Sykes kilichotokea jana Jumapili ya Tarehe 15/02/2015.
Pamoja na vifo hivi kuacha majonzi na huzuni kwa wanafamilia, ni pigo pia kwenye tasnia ya Sanaa kutokana na ukweli kwamba wote wawili kwa njia moja ama nyingine wamekuwa na mchango katika kuhakikisha tasnia hii inasonga mbele kwa kuwa karibu na wasanii John Kitime na Dully Sykes sawia.
Baraza linatoa pole kwa wadau wote wa Sanaa hususan wasanii na Umoja wa mabloga nchini kwa misiba hii. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu hawa hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...