Mkuu wa Biashara za Kimtandao wa Copy Cat Tanzania Limited,Jonnavithola Prasad akizungumza na waandishi wa habari juu uzinduzi wa kifaa cha kuzuia wizi wa mtandao na jinsi walivyojipanga katika kutoa ushauri wa kifaa hicho katika hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam jana.
Mshauri wa Teknolojia na Biashara wa Copy Cate Tanzania Limited, Nathalie Ayonga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya uzinduzi wa kifaa cha kuzuia wizi wa mtandao, hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam jana.
Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii.
Kampuni ya Copy
Cate Tanzania Limited wamezindua mfumo wa kuzuia wizi katika mtandao ambao una
uwezo mkubwa wa kuzuia kwa mtu mmoja mmoja au kundi lililo katika mtandao
mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika
ukumbi wa Hoteli Hyatt Regency,Jijini
Dar es Salaam,Mshauri wa Masuala ya Teknolojia ,Biashara,Naththalie Ayonga ,alisema
mfumo huo katika mitandao utasaidia
taasisi za serikali sekta binafsi na mtu mmoja moja kuweza kudhibiti wizi wa taarifa katika mitandao.
Ayonga
alisema kampuni imekuwa ikifanya kazi za mafanikio katika mfumo wa mabadiliko
wa teknolojia kwa kuweza kufanya ingiaji wakati uzinduzi wa kimfumo katika
karne ya 21 ya sayansi na Teknolojia.
Alisema
kifaa hicho cha kuzuia wizi wa taarifa katika mitandao wa mfumo huo kimekuja kwa wakati mwafaka kwa
Tanzania kutokana na kuwepo watu wengi kuingia katika teknolojia za mitandao
bila kuwa na ulinzi.
Kifaa cha
mfumo kinajulikana kama Cisco ambacho kimekuwa na chachu kudhibiti wizi katika
mitandao hivyo ni fursa ya watazania kupokea katika kulinda taarifa zao
zisiingiliwe na mtu mwingine.
Kampuni ya Copy
Cat Tanzania Limited ndio itakuwa inafanya
masuala ya kifumo katika mitandao na uingizaji wa bidhaa mpya na ambayo ilikuwa ikifanyw na BMTL.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...