Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Mradi huu utakapokamilika na kupokelewa na Serikali Mkandarasi atakaa site miaka mitatu kwa ajili ya uangalizi na kufanya marekebisho yoyote yatakayojitokeza kwa gharama zake mwenyewe.
. Sehemu ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye jumla ya km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii imekamilika kujengwa kwa asilimia 97.
Sehemu unapojengwa mzani utakaotumika kupimia magari makubwa yatakayopita kwenye barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itigi waliofika kumpokea kabla ya kuwahutubia wananchi kuhusu maendeleo ya mradi huo wa barabara. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Hiyo barabara italeta maendeleo makubwa sana, kwa kweli nakupongeza Mh Magufuli na wenzako waliobuni mradi huu.
ReplyDeleteNilipopita kabla ya kumalizika barabara hii nilidhani bado hilo eneo liko katika himaya ya Tanganyika kwa vile lilivyo, yaani walikuwa nyuma kama miaka 150 hivi.