Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. John Pombe
Magufuli amelaani vikali tukio la kikatili la kutekwa na kuuawa kwa
mtoto Yohana Bahati pamoja na kujeruhiwa vibaya kwa mama mzazi wa
marehemu na watu wasiofahamika.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa jijini Dar es Salaam, Dkt.Magufuli
amewataka Watanzania kuishi kwa amani na upendo na kuacha dhana ya
kutajirika kutokana na viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino).
“Tukio hili ni la kinyama na halikubaliki popote Duniani, watu wanatakiwa
waelewe kuwa mtu huwezi kutajirika kutokana na viungo vya watu wenye
ulemavu wa ngozi kama alivyofanyiwa mtoto Bahati” Alisema Waziri
Magufuli.
Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli ametoa msaada wake wa awali
kiasi cha Shilingi milioni Moja kwa ajilili ya kumsaidia Ester Jonas mama
mzazi wa mtoto huyo aliyeuawa na watu hao wasiofahamika.
“Nimeona nitoe msaada wangu wa awali kiasi hichi cha fedha kwa ajili
ya kumsaidia mama huyu aliyejeruhiwa vibaya kwa ajili ya mahitaji yake
mbalimbali na hapo badae ntakapopata nafasi ntakwenda nyumbani kwake
kutoa pole zaidi”
Aidha, Waziri Magufuli ameishukuru Hospitali ya Wilaya ya Chato pamoja
na Bugando kwa msaada mkubwa wa kumpatia matibabu mama huyo
aliyejeruhiwa vibaya na watu hao wasiofahamika.
Pia Waziri Magufuli aliipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Geita kwa kazi kubwa ya kuwatafuta wale wote waliohusika na tukio hilo la
kikatili.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Chato mkoani Geita Dkt. John Pombe Magufuli(kushoto) akikabidhi
msaada wa fedha Shilingi Milioni Moja kwa Mwandishi wa ITV Ndugu
Emanuel Buhohela(kulia) kama mchango wake wa awali kwa ajili ya
kumsaidia Ester Jonas aliyejeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika wakati
wa tukio la kutekwa kwa mwanaye mwenye ulemavu wa ngozi(Albino)
Yohana Bahati aliyeuwawa katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Mama
huyo bado amelazwa katika katika Hospitali ya Bugando kwa ajili ya
matibabu. Habari na Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Ujenzi
Ma engineer. Wa jiji acheni kukaa ofisini na fanyeni kazi sio mnakaa tu ujenzi karibu wote. Unayofanyika sasa na makarandasi iko chini ya kiwango mnagojea mpaka Ajali itufikiye. Mheshimiwa slaa watu wako. Hawafanyi kazi zao fanya mabadiliko
ReplyDelete