Mfuko wa Pensheni wa GEPF umesaini mkataba wa uwekezaji na Bodi
ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika eneo la Bunju.  Uwekezaji huo 
utakaohusisha kumbi za mikutano (Conference Halls) zenye uwezo wa 
kuchukua watu Zaidi ya 1,200, migahawa (Restaurants), Hoteli yenye 
hadhi ya kimataifa yenye vyumba Zaidi ya 102, Maktaba, Bwawa la 
kuogelea (Swimming Pool) pamoja na sehemu za mazoezi (Gymnasium)
Uwekezaji huo utagharimu Zaidi ya shilingi Bilioni 33 za kitanzania na 
unategemewa kukamilika katikati ya mwaka huu 2015.
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia) akiongoza majadiliano
ya awali kati ya Menejimenti ya GEPF pamoja na Menejimenti ya NBAA 
kabla ya zoezi la kutiliana saini mkataba wa uwekezaji.
Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF,Bi. Joyce Shaidi (kulia) pamoja na mwenyekiti
wa NBAA Profesa Issaya Jairo wakisaini mkataba wa ushirikiano wa 
uwekezaji wa pamoja wakiongozwa na mwanasheria wa NBAA Bi 
Agness Kessy.
Utiaji saini huo ulishuhudiwa na makamu mwenyekiti wa NBAA Bi
Anna Mbughuni ( mwenye suti ya blue), Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA 
Bw Pius Maneno,  Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi pamoja 
na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GEPF Bw Festo Fute.
Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF Bi Joyce Shaidi akibadilishana nyaraka
za mkataba wa uwekezaji wa pamoja  na Mwenyekiti wa NBAA Profesa 
Issaya Jairo.
Pichani baadhi ya watendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi
(NBAA) wakifurahia jambo mara baada ya zoezi hilo kukamilika.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...