1Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua mchango wake akiwa mwanzilishi wa mfuko huo wakati wa hafla ya kuwaaga viongozi na wafanyakazi wastaafu iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki , Mzee Emannuel Humba aliwaasa wafanyakazi wa mfuko huo kushikamana na kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha mfuko huo unafikia malengo, Katika hafla hiyo Emanuel Humba pia amezawadiwa zawadi mbalimbali. wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bw. Michael Mhando.2Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akitoa shukurani zake kwa uongozi wa NHIF na wafanyakazi kwa ujumla kwa kuwaadalia hafla hiyo ya kuwaaga. 3Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akipokea shada la maua kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF. 6
Dr Marqus Kalinga Mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akipokea tuzo yake kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Balozi Ali Mchumo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Michael Mhando.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...