
Na Mwandishi wetu, Addis Ababa
Kampuni
ya Huawei Technologies inayoongoza katika sekta ya habari na
mawasiliano duniani, imesaini makubaliano (MoU) na Umoja wa Afrika (AU),
makubaliano yatakayosaidia kuongeza ushirikiano baina yao katika
kuimarisha maendeleo katika miundombinu ya teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (teknohama).
Makubaliano
hayo yalisainiwa hivi karibuni mjini Addis Ababa, Ethiopia kwenye
Mkutano wa AU wa mwaka 2015 ambao pamoja na mambo mengine ulijadili pia
namna ya kuimarisha uelewa wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(teknohama) kwa nchi wanachama sambamba na kujenga uwezo wa juu katika
maendeleo ya miundombinu ya teknolijia hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Makamu mweyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Erastus Mwencha alisema maendeleo ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (teknohama) yana msaada mkubwa kwa ukuaji wa
uchumi ulimwenguni na pia ni nguzo muhimu katika kuleta madadiliko
chanya kwenye setka mbalimbali.
“Maendeleo
ya teknolojia hii yataleta mabadiliko makubwa sana katika sekta
mbalimbali na ndio maana tunatafuta washirika wanaoweza kufanya kazi na
sisi ili kufanikisha hilo. Huawei kama kampuni imara kwenye teknolojia
hiyo tunaamini pia itakuwa ni msaada mkubwa itakapo shirikiana na
sisi...tunafurahi kuwa nao kwenye huu mradi,’’ alisema Mwencha.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa
kampuni ya Huawei katika idara inayohusika na mahusiano ya serikali
Ulimwenguni, Bw. David Harmon alisema kampuni yake ina nia
yakukuza kimataifa maendeleo sekta ya teknohama na ndiyo maana kwa
muda mrefu imekuwa ikisaidiana na serikali mbalimbali katika kuimarisha
miundombinu inayohusiana na sekta hiyo.
“Huawei ina
jukumu la kuhakikisha tunashikirikaina na washirika wetu kwenye nyanja
zote za teknohama ili kujenga Afrika bora yenye kushikamana, kwa sababu tunaamini kwamba teknolojia ICT, hasa mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu si tu kwa Afrika bali ulimwenguni wote.
"Kwa
miaka yetu 17 ya uzoefu katika sekta ya teknohama sambamba na mtandao
wa kimataifa ulimwenguni kote ina maana kwamba Huawei ipo katika
nafasi nzuri ya kushiriki kwenye namna bora ya kutafuta ufumbuzi kwa
masuala ya teknohama. Tupo tayari kubadilishana uzoefu wetu na Umoja wa
Afrika, " Harmon aliongeza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...