Na Bashir Yakub
Wapo
watu ambao baada ya kupata cheo au
nafasi ya kuwa wasimamizi wa mirathi hugeuka waungu.
Huwa hawaambiwi wala hawasikii
la mtu. Huwezi kuamini kuwa
kuna baadhi ya wasimamizi wa
mirathi wamekataa kugawa
mali za marehemu sasa ni zaidi ya miaka kumi. Na
si kwamba wamefanya hivyo kwa maslahi mapana ya familia, hapana. Wamefanya hivyo kwa ukorofi lakini kubwa zaidi wanafanya hivyo
ili waendelee kunufaika na mali za marehemu peke
yao. Mambo hayo yameleta sana
faraka kwenye familia.
Warithi na wote wenye haki katika mali za
marehemu wengi wao huchukizwa na matendo
haya yumkini wapo ambao hujua
la kufanya na wapo ambao hubaki njia panda wasijue la kufanya. Mali zinaliwa
lakini warithi wafanye nini, hawaoni njia. Katika makala haya nini
mfanye iwapo hamridhishwi au hamumtaki kabisa msimamizi wenu wa mirathi ni kati ya mambo
yatakayoguswa.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...